Urambo. Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imeiagiza
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, kuwalipa fidia ya Sh25 milioni Mwamini
Adam na mumewe Idrisa Jafari kutokana na madhara waliyopata baada ya
uzembe uliofanywa na daktari wa Hospitali ya wilaya hiyo alipokuwa
akimfanyia upasuaji Mwamini.
Katika uamuzi wa shauri hilo la madai Namba
13/2011 uliotolewa juzi, Mahakama Kuu imeiagiza halmashauri hiyo kumlipa
Sh20 milioni Mwamini aliyepata kilema cha maisha kwa kuondolewa mfuko
wa uzazi na kukatwa utumbo.
Pia, mahakama imeiagiza halmashauri hiyo kumlipa
fidia ya Sh5 milioni Jafari ikiwa ni gharama za uendeshaji wa shauri hilo.
fidia ya Sh5 milioni Jafari ikiwa ni gharama za uendeshaji wa shauri hilo.
Akisoma hukumu, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu
Kanda ya Tabora, Amir Mruma alikubaliana na madai ya walalamikaji kuwa
madhara waliyopata kutokana na uzembe uliofanywa na Dk Jackob Kamanda ni
makubwa.
Jaji Mruma alisema haipingiki kwamba huo ni uzembe uliofanywa na mtumishi, hivyo mwajiri anapaswa kulipa gharama.
Aliagiza kuwa kiwango hicho cha fedha kitalipiwa
riba ya asilimia saba kila siku kuanzia tarehe ya uamuzi ulipotolewa
hadi siku mlalamikiwa atakapolipa fedha hizo.
Mwamini na mumewe walifikisha malalamiko yao
Mahakamani Kuu, wakidai kulipwa fidia ya Sh505 milioni kutokana na
makosa ya uzembe uliofanywa na wataalamu wakati wa upasuaji kwa kuacha
kitambaa tumboni mwa mgonjwa.
Wakili wa walalamikaji, Jaji Mussa Kwikima aliiambia Mahakama kuwa uzembe huo umemsababishia kilema cha maisha mteja wake.
Awali, akiwaongoza wateja wake kutoa ushahidi,
Wakili Kwikima, waliieleza Mahakama kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji,
Mwamini alihamishiwa Hospitali ya Rufani Kitete, lakini hali ilizidi
kuwa mbaya ikawalazimu kuhamia Hospitali ya Itigi kulikogundulika tatizo
baada ya vipimo.
Walidai kuwa madaktari walibaini kuwa kulikuwa na
kitu ndani ya tumbo la Mwamini kilichokuwa kinasababisha atokwe na usaha
sehemu za siri na tumboni.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Anatory
Lukonge wa Hospitali ya Itigi ambaye alimfanyia upasuaji Mwamini katika
ushahidi wake, aliieleza mahakama kuwa walipomfanyia upasuaji walikuta
utumbo umeshikana na kizazi huku juu yake kukiwa na kitambaa.
Dk Lukonge alisema walikitoa kitambaa hicho lakini
kutokana na sehemu ya kizazi kuharibika, iliwalazimu kukiondoa huku
akidai kuwa hali hiyo ilisababishwa na uzembe wa daktari aliyemfanyia
upasuaji
0 comments:
Post a Comment