Mashabiki wa soka kesho watawashuhudia wachezaji wa zamani wa timu ya Barcelona ya Hispania, Patrick Kluivert, Gaizka Mendieta, Anderson de Sousa “Deco” Francesco Coco na Luis Garcia wakionyeshana kazi na wakali wa Tanzania kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Watanzania kushuhudia mastaa hao wa zamani wakikipiga kwenye uwanja huo baada ya wale wa Real Madrid waliokuwa chini ya Luis Figo, Christian Karembeu na Fabio Cannavaro wakicheza kwenye uwanja huo kwa mara ya kwanza na kushuhudiwa na Rais Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikosi cha FC Barcelona kimesheheni wachezaji nyota wengi mbali ya Kluivert na wenzake ambao kwa mashabiki wa soka ni majina maarufu. Wachezaji wengine ambao wanatarajia kushuka leo uwanjani chini ya kocha maarufu, Johan Cruyff ni pamoja na makipa nyota, Jesus Mariano Angoy Gil na Robert Oscar Bonano.
Wengini ni Sergi Barjuan Esclusa, Albert Toams Sobrepera, Luis Milla Aspas, Lluis Carrreras Ferrer, Miguel Angel Nadal Homar, Ion Andoni Goikoetxea Lasa, Oscar Arpon Ochoa, Santiago Ezquerro Marin, Javier Villena Mulero, Magin Civantos Martinez, Mateo Segura Capellades na Simao Sabrosa.
Kocha wa timu hiyo, Cruyff alisema kuwa wamekuja kuonyesha vipaji vyao vya zamani vilivyotukuka na hakuna wa kuwazuia kushinda katika mechi hiyo. Alisema kuwa wachezaji wake wegi japo wameacha soka, bado wanajihusisha kwa kufundisha na wengine kufanya mazoezi kwa ajili ya timu yao “FC Barcelona Legends”.
“Tupo vizuri, tumejiandaa kwa ajili ya kuweka historia, tunajua wenyeji wataleta upinzani, lakini sisi ndiyo tutakuwa washindi,” alisema Cruyff kwa kifupi.
Mratibu wa mechi hiyo kutoka kampuni ya Primetime Promotion, Stuart Kambona alisema kuwa maandalizi yamekamilika na kikosi cha Tanzania Stars kitakuwa na nyota kama Manyika, Kaseja Shadrack Nsajigwa, Abubakari Kombo, Mustapha Hozza, Salvatory Edward, Amour Aziz, na Yusuph Macho.
Wengine kwa mujibu wa Kambona ni Shaban Ramadhan, Dua Saidi, Nassoro Bwanga, Mohamed Hussein, Steven Nyenge, Mwanamtwa Kihwelu, Edibily Lunyamila, Henry Morris, Haruna Moshi, Bitta John, Madaraka Selemani, Deo Lucas, Bakari Malima, Thomas Kipese, Khatibu Sinapo na Nico Nyagawa.
Kambona alitaja viingilio katika mchezo huo kuwa ni Sh 7,000 kwa viti vya kijani, Sh10,000 (blue), Sh20,000 (Orange), Sh30,000 (VIP C), Sh50,000 (VIP B) na SH300,000 for VIP A.
Kocha wa magwiji wa Barcelona Johan Cryuff mwenye shati nyeupe akishuka kwenye ndege ya serikali tayari kwa mechi dhidi ya magwiji wa tanzania itakayopigwa kwenye uwanja wa taifa.
Mchezaji wa zamani wa Liverpool na Barcelona, Luis Garcia mwenye fulana nyeupe akishuka kwenye ndege
Msafara wa wachezaji na viongozi wa hotel ya Ledger Plaza bahari beach wakiwa na wachezaji wa barcelona wakielekea kwenye chumba maalum tayari kuzungumza na waandishi wa habari
Meneja mkuu wa hotel ya Ledger Plaza bahari beach, Wissem Souifi (mwenye tai) akibadilishana mawazo na kocha wa barcelona Johan cryuff huku wakielekea kwenye mkutano na waandishi wa habari
Luis garcia ( kulia) akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari. wengine katika picha ni Kocha Johan Cryuff (katikati) na kiungo machachari, Gaizka Mendieta
0 comments:
Post a Comment