Hii ni Ripoti ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomezaaliyopokea Raisi Kikwete
- Mwenyekiti
wa Tume ya Uchunguzi kuhusu operesheni tokomeza Jaji(Mstaafu) Balozi
Hamisi Amiri Msumi akimkabithi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ripoti ya
Uchunguzi wa Tume hiyo katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar
es Salaam leo.Rais Kikwete aliiteua tume hiyo mwaka jana kuchunguza
tuhuma za uvunjifu wa sheria katika utekelezaji wa operesheni hiyo
- PRESIDENT’S OFFICE,
- STATE HOUSE,
- 1 BARACK OBAMA ROAD,
- 11400 DAR ES SALAAM.
- Tanzania.
- TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
- Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Ijumaa, Aprili 10, 2015 amepokea Ripoti ya Uchunguzi wa Operesheni
Tokomeza katika halfa fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam.
- Mara
baada ya kupokea Ripoti hiyo, Rais Kikwete ameishukuru Tume kwa kazi
nzuri na kuongeza kuwa amefurahi kuwa suala zima la Operesheni Tokomeza
sasa limefika mwisho wake.
- Aidha,
Rais amesema kuwa Serikali itaisoma Ripoti hiyo na katika wiki mbili
itatoa maelezo ya jinsi Ripoti hiyo itakavyoshughulikiwa.
- Rais
Kikwete amepokea Ripoti hiyo kutoka kwa Balozi Jaji (mstaafu) Hamisi
Amiri Msumi, Mwenyekiti wa Tume ambayo Rais Kikwete aliiteua Mei Mosi,
mwaka jana, 2014, na kuitaka ichunguze tuhuma mbali mbali za uvunjifu wa
Sheria, Kanuni, Taratibu na Hadidu za Rejea za Utekelezaji wa
Operesheni Tokomeza.
- Aidha,
Rais Kikwete aliipa Tume hiyo jukumu la kupendekeza hatua stahiki za
kisheria za kuchukua dhidi ya watakaobainika kuhusika na uvunjifu huo.
Vile vile, Rais aliiagiza Tume hiyo ishauri namna bora ya utekelezaji wa
Operesheni kama hiyo hapo baadaye.
- Rais
Kikwete pia aliipa Tume hiyo Hadidu za Rejea sita ambazo pia
ziliainishwa katika Taarifa ya Serikali Nambari 131 ya 2014. Hadidu za
Rejea hizo ni kama zifuatazo:
- (a) Kuchunguza namna Operesheni Tokomeza ilivyotekelezwa;
- (b)
Kuchunguza iwapo maafisa waliotekeleza Operesheni Tomokeza
walizingatia sheria, kanuni, taratibu na hadidu za rejea walizopewa;
- (c)
Kuchunguza iwapo maofisa waliotekeleza Operesheni Tokomeza
walivunja sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea walizopewa.
- (d)
Kuchunguza iwapo kuna watu waliokiuka sheria yoyote wakati wa
utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na iwapo hatua zilizochukuliwa na
maofisa wa Operesheni Tokomeza dhidi ya wakosaji hao na mali zao
zilikuwa sahihi;
- (e)
Kupendekeza hatua zinazostahili kuchukuliwa dhidi ya maafisa
wa Operesheni Tokomeza waliokiuka sheria, kanuni, taratibu na hadidu za
rejea za Operesheno Tokomeza; na
- (f)
Kupendekeza mambo yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa kupanga
na kutekeleza Operesheni nyingine kama hii, ili kuepuka malalamiko
mengine yasitokee.
- Jaji
Msumi amemweleza Rais Kikwete kuwa katika kutelekeza majukumu yake,
Tume ilitembelea mikoa 20 na wilaya 38 na kupokea malalamiko mbali mbali
kutoka kwa wafuatao:
- (a) Viongozi wa Serikali ikiwa ni pamoja na mawaziri wanne waliojiuzulu kutokana na sakata hilo;
- (b) Watekelezaji wa Operesheni; na
- (c) Walalamikaji/wahanga wa Operesheni.
- Jaji
Msumi amemweleza Rais Kikwete kuwa Ripoti ya Tume ina Juzuu kumi, Juzuu
ya kwanza ikiwa ni Muhtasari wa Taarifa ya Tume, Juzuu ya pili ikiwa ni
Taarifa yenyewe ya Tume, Juzuu ya tatu hadi ya tisa ikiwa ni Mwenendo
wa Ushahidi (Proceedings) na Juzuu ya kumi ikiwa ni vielelezo
vilivyotolewa na mashahidi.
- Mwisho.
- Imetolewa na;
- Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
- Ikulu – Dar es Salaam.
- 10 Aprili, 2015
- Rais
Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Uchunguziwa
operesheni Tokomomeza ikulu leo.(picha na Freddy Maro.
0 comments:
Post a Comment