Enugu, Nigeria. Mchungaji Timothy Ngwu
(53) wa nchini Nigeria amewapa mimba zaidi ya waumini wake 20 kwa madai
ya kwamba Roho Mtakatifu alimwabia afanye mapenzi nao.
Kiongozi huyo wa kanisa la Vineyard
Trinity ambaye hivi sasa anashikiliwa na polisi nchini humo, alifanya
kitendo hicho kwa waumini wanawake ambao wameolewa na wasichana wadogo
ambao hawajaolewa.
Akizungumza na gazeti la NAIJ na baadaye
kunukuliwa na gazeti la Jewsnews la nchini humo, Msemaji wa Kituo cha
Polisi cha Enugu ambapo Ngwu anashikilikiwa, Ebere Amaraizu alisema
wamemkamata kiongozi huyo kwa kosa la unyanyasaji wa kijinsia kwa
waumini wanawake.
“Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba
alilazimika kufanya hivyo kwani hayo yalikuwa maono ya kinabii na
alifanya hivyo kwa sababu alikuwa anatii maono aliyoonyeshwa na Mungu.
Maono ambayo ni kumpa mimba mwanamke yeyote ambaye Mungu amemchagua na
kumwonyesha yeye kwa njia ya Roho Mtakatifu bila ya kujali kama huyo
ameolewa au la,”alisema Amaraizu.
Aliongeza: “Mwanamke akijifungua atakuwa akiishi kanisani pamoja na mtoto kwa maisha yao yote.”
Mke wa mchungaji huyo ambaye baadaye
alimfukuza, Veronica Ngwu ndiye aliyeenda kutoa taarifa katika kituo cha
polisi baada ya kuchoshwa na tabia hiyo hasa alipofikia hatua ya kumpa
mimba mtoto wa kaka yake.
Ndugu wa karibu wa mchungaji huyo ambaye
hakupenda jina lake litajwe alisema walimuonya kaka yao juu ya tabia
hiyo, lakini hakutaka kuwasikiliza huku akidai kuwa anatekeleza agizo la
Mungu.
“Hiki kilichompata kaka yetu ni hasira
kutoka kwa Mungu kwa sababu tulimuonya lakini hakutaka kutusikiliza.
Amekuwa mtemi hapa kwetu, anawapa wanawake mimba hovyo hovyo kwa kutumia
jina la Mungu halafu ukimuonya anasema tunamuonea wivu,”alisema.
Alilalamika kuwa, Ngwu amejimilikisha
sehemu ya shamba la familia yao na kufanya kanisa lake ambalo anatumia
kwa kufanyia maovu hayo kwa jina la Mungu.
“Alimfukuza mke wake ambaye amezaa naye
watoto watatu halafu sasa hivi anafanya kazi ya kuzaa na kila mwanamke
bila kujali kama ameolewa au hajaolewa wengine ni wasichana
wadogo…angalia uwanja mzima umejaa watoto wa umri na jinsia tofauti,
“alilaumu.
Ndugu huyo alisema, inashangaza kuona mtu na elimu yake anafanya vitendo kama hivyo.
0 comments:
Post a Comment