MPIGANIA UKOMBOZI WA AFRIKA KUSINI ALIYEMTOA MANDELA GEREZANI BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA AFARIKI DUNIA

Leave a Comment


 Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), amefariki dunia asubuhi ya tarehe 26 Aprili 2015 katika hospitali kuu ya Jeshi, Lugalo,  jijini Dar es salaam. 

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Chang'ombe jirani na TCC Club jijini Dar es salaam.

Mzee Mbita atakumbukwa Tanzania,  bara zima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni  barani Afrika, hususan utawala kidhalimu wa makaburu  Zimbabwe na  Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa Nelson Mandela.
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment