Shule 250 za Serikali Kuunganishwa na Intanet

Leave a Comment



Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote imesaini mkataba na Kampuni za Mawasiliano kwa ajili ya kuziunganisha shule 250 za Serikali na intaneti pamoja na kuanzisha vituo 25vya kuwafundishia walimu.Utekelezaji wa mradi huo wa mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kwa kuunganisha shule, unategemewa kukamilika ndani ya mwaka huu.



Hayo yalibainishwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alipokuwa akizungumza na wadau na Kampuni za mawasiliano nchini.Waziri Mbarawa alisema katika kipindi cha mwaka jana, Kampuni za simu za Voda na Tigo, hazikukamilisha ujenzi wa mawasiliano waliokubaliana katika zabuni walizopewa hivyo aliagiza kampuni hizo, kukamilisha ujenzi huo katikakipindi hiki licha ya kwamba wameshafunga mkataba wao mwaka uliopita.



Pia alisema kuwa kuna maeneo nchini, ambayo mpaka sasa yana matatizo ya mawasiliano na kwamba wameingia mkataba na kampuni zote za mawasilianoTigo, Voda, Airtel na TTCL ili kuhakikisha tatizo hilo linatoweka.‘’Pamoja na mambo mengine,leo pia tumesaini mkataba wakupeleka mawasiliano vijijini katika Kata 102 mradi wa awamu ya pili A (2A) ambapo ruzuku ni Sh bilioni 14.2 na kata 10 za mradi wa mawasiliano mipakani na maeneo maalumu ruzuku ni Sh bilioni 2.7,’’alisema Profesa Mbarawa.


Akizungumzia fursa ya wazawa katika ununuaji wa hisa zinazotolewa na kampuni za mawasiliano, Waziri huyo alisema kuwa wameshaandaa kanuni ambazo zitawasaidia wazawa kuweza kuingia katika ununuaji wa hisa, ili kuhakikisha Kampuni za mawasiliano nchini hazirudi nyuma katika kutoa huduma.




Alisema kuwa kanuni hizo zinatarajiwa kutangazwa ndani ya mwaka huu na kwamba wataangalia jinsi ya kuwawezesha wazawa kufanikiwa pamoja na kuongeza mitaji kwa kampuniza mawasiliano kupitia hisa hizo.“Serikali imeshirikiana na Benki, Soko la hisa Dar es Salaam, Kampuni za simu kuandaa kanuni hizo ambazo zitasaidia kuhakikisha wanakua kimaendeleo na sio kushuka kiuchumi,’’alifafanua.



Aliongeza kuwa ipo haja ya Watanzania wenyewe kuhakikisha wanakuwa mstariwa mbele katika kununua hisa ili wasiwe na kisingizio cha kwamba wageni ndio wananufaika na hisa zinazotangazwa.‘’Kama tusipokuwa makini ni lazima tutaona kuwa wageni wananufaika na hisa zinazotangazwa. Hivyo tunaandaa kanuni ili kuhakikisha na wazawa wanakuwa mstari wa mbele kununua hisa hizo,’’alisema.
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment