Kundi
zima la Yamoto Band punde walitinga Katika Kituo cha Radio Kasibante
88.5 Bukoba kuongea moja kwa moja na Wakaazi wa Bukoba juu ya Shoo ya
yao inayotarajiwa kufanyika Usiku huu katika Ukumbi wa Burudani wa
Lina's Night Bukoba. Bendi inayokuja kasi hapa Nchini inayoundwa na
Vijana Machachari kama Aslay, Becka, Bella na Maromboso wameteta na
Wanabukoba kwamba waje kwa wingi katika Ukumbi huo wa Lina's wajionee
walichokuja nacho kipya katika Pasaka hii ya pili maana kwa sasa
watawasha Moto wa Uhakika na Watatoa Burudani Live jukwaani na wamekuja
wamejipanga wakiwa na Vijana wengine ambao ni Maalum kwa Kuliteka Jukwaa
kwa mapigo ya Live"
Mtandao
huu wa jamii murua kwa habari tamu za Michezo na Burudani pia umeweza
kuzinyaka za haraka haraka kwamba baada ya Shoo ya leo katika Ukumbi wa
Lina's Kesho Jumatatu watatoa Burudani pia huko Biharamulo kwa kiingilio
cha 10,000/ siku ambayo ni Karume Day" ya jumanne tarehe 07/04/2015.
Kiingilio cha Shoo ya leo ya Lina's kwa kawaida ni Tsh 10,000/ na VIP ni
Tsh.15,000/-
0 comments:
Post a Comment