Filamu mpya ya 'Sio Dili' Inayoongelea Tatizo la Mauaji ya Albino Kuingia Sokoni hivi karibuni

Leave a Comment
Filamu ya 'Sio Dili' Inayoongelea Tatizo la Mauaji ya Albino Kuingia Sokoni
Kampuni ya K Films Production ya jijini Dar es Salaam inatarajia kuachia filamu kali na ya kusisimua ya Sio Dili inayoongelea tatizo la mauaju ya Albino Tanzania ambayo yanatikisa nchi nzima, akiongea na FC amesema kuwa sinema hiyo ni funzo.
“Filamu ya Sio Dili ni kazi yangu katika harakati za kupambana na mauaji ya Albino ambayo yanahusisha imani ya kishirikina ni kazi nzuri inayoelimisha jamii kuachana na imani potofu,”anasema Kinye Mkali.
Sinema hiyo inawashirikisha wasanii nyota kama Mohamed Fungafunga ‘Mzee Jengua’ Mobby Mpambala, Master Jumanne, Port Lee, Ben Blanco na kijana Albino Samson Samwel Makoba ‘Sammy White.
Sammy White ni kijana mwenye kipaji kutoka Mkoani Mara kinara wa filamu ya Sio Dili anayepambana na watekaji wa Albino, sinema hiyo inaingia sokoni wiki ijayo na kusambazwa na KFP Media Station.
Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment