CHADEMA imeonesha dalili tatu za wazi za kujiengua kutoka kwenye umoja huo kabla ya kufikia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatatu ya Oktoba 25, mwaka huu baada ya kuanza kufanya maandalizi ya uchaguzi huo kivyake na kutofautiana kimsimamo juu ya kujiunga kwa chama cha siasa cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Zuberi Kabwe.
Dalili ya kwanza ya CHADEMA kujiengua kwenye UKAWA ambao ni umoja shinikizi wa kikatiba ulioanzishwa Februari mwaka jana, kwa kuvihusisha vyama vyingine vya CUF, NLD na NCCR-Mageuzi ni kushindwa kuheshimu utaratibu mpya wa kuachiana na majimbo ya uchaguzi.
Hilo linatokana na ukweli kwamba, chama hicho imeanza mchakato wa kuorodhesha wanachama wake wasomi wanaotaka kuwania ubunge na udiwani kwenye maeneo mbalimbali bila kujali kwamba maeneo hayo kuna wabunge wa vyama vingine kama vitasimamisha mgombea kwenye maeneo hayo au la.
Chanzo: Taifa Imara
0 comments:
Post a Comment