Rais Zuma amechukua hatua hiyo kufuatia kuuliwa raia kadhaa wa
Msumbiji, katika vurugu zilizoambatana na mashambulizi dhidi ya raia wa
kigeni nchini humo na kuongeza kuwa, kitendo hicho ni cha kusikitisha
mno.
Rais Zuma amesema kama ninavyonukuu: "Raia wa Msumbiji ni ndugu
zetu na wananchi wa nchi mbili ni watu wa familia moja." Mwisho wa
kunukuu.
Aidha rais huyo wa Afrika Kusini ameahidi kutojikariri tena
mashambulizi dhidi ya wahajiri wa kigeni nchini mwake huku akiahidi pia
kuwachukulia hatua kali wahusika wa vitendo hivyo.
Itakumbukwa kuwa
mnamo tarehe 21 April mwaka huu, Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji aliitaka
serikali ya Pretoria kuhitimisha mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni
nchini humo. Inaelezwa kuwa, raia kadhaa wa Msumbiji walipoteza maisha
katika vurugu hizo huku wengine wakipoteza vitu vyao vya thamani.
Katika
hujuma hizo, makumi ya raia wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali hususan
ya Afrika waliuawa na raia wa Afrika Kusini waliokuwa na hasira kali
wakiwatuhumu wageni hao kuwa chanzo cha wao kukosa ajira.
0 comments:
Post a Comment