Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akilihutubia Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete na Spika wa Bunge hilo Mh.Anna Makinda wakisikiliza.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania
Mh.Anna Makinda akimkaribisha Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi katika
viwanja vya Bunge mjini Dodoma ambapo Rais huyo alilihutubia Bunge hilo.
Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akipokea
heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma
akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akisaini
kitabu cha wageni ofisini kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
leo huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika Mhe.Anna Makinda wakishuhudia.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto
Nyusi,Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na viongozi waandamizi katika serikali ya Msumbiji wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya Rais wa Msumbiji kulihutubia Bunge
lao mjini Dodoma.
(Picha na Freddy Maro)
0 comments:
Post a Comment