Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mh. Fadhil Nkurlu (kushoto) akimhoji dereva
wa lori aliyejitambulisha kwa jina la Kabyemela (mwenye tisheti nyekundu)
baada ya kuwekewa mtego na kukamatwa na shehena ya ngozi ya magendo
iliyokuwa ikisafirishwa kuelekea nchi jirani. Shehena hiyo ilikamatwa
katika kizuizi cha Kyaka.
Baadhi ya ngozi ya magendo iliyokamatwa na Mkuu huyo wa Wilaya baada ya kuweka mtego kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama. Shehena
hiyo ya ngozi ya magendo inakisiwa kufika uzito wa takribani tani 10.
Missenyi. 8 Mei, 2015 - Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mh.
Fadhil Nkurlu amekamata shehena kubwa ya ngozi ya magendo yenye uzito
unaokisiwa tani 10 ikisafirishwa kwenda nje ya nchi bila kibali wala
nyaraka zozote za serikali.
Kutokana na
taarifa za ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Missenyi ngozi hiyo ilitokea
Kahama ikiwa inaelekea nchini Uganda na ilikamatwa katika kizuizi cha
Kyaka, wilayani Missenyi.
"Tulipata taarifa
kutoka kwa raia wazalendo tangu jana yake kwamba kuna bidhaa za magendo
ambayo huwa yanapita usiku, ndipo nikawapanga vijana kutoka vikosi vyote
vya ulinzi na usalama kuweka mtego huu," alisema DC Nkurlu.
"Hiki
ni kipindi ambacho magendo ya kahawa husafirishwa kwa wingi kwenda nje
ya nchi na hivyo hukosesha serikali mapato yake stahiki. Lakini
tumejipanga ipasavyo na tutahakikisha tunakamata kila aina ya magendo.
Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayejihusisha katika
biashara hii," alisisitiza.
"Napenda kutoa rai
kwa wananchi wote wa Missenyi kuendelea kutoa ushirikiano wao kwa
serikali ili kuweza kukamata bidhaa hizi za magendo na kudhibiti mtandao
huu haramu," alisema Mh. Nkurlu.
Hii ni mara
ya pili ndani ya wiki hii magendo yanakamatwa ambapo Jumatatu shehena
kubwa ya mbao zilikuwa zikisafirishwa kinyemela zilikamatwa na bado
zinashikiliwa katika kituo cha polisi cha Kyaka.
0 comments:
Post a Comment