Robo
fainali ya michuano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe la
Kagame inaanza hapo kesho kwa kuzikutanisha timu ya APR na Khartoum
ukifuatiwa na Gor Mahia watakaocheza dhidi ya Malakia uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Kizuguto amesema, robo fainali ya pili itafanyika hapo Jumatano kwa kuzikutanisha wenyeji Yanga na Azam FC ukitanguliwa na mchezo kati KCC dhidi ya Al Shandy Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku nusu Fainali ikitazamiwa kuchezwa siku ya Ijumaa huku fainali ikichezwa Jumapili ikitanguliwa na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.
Kwa upande mwingine Kizuguto amesema, Kamati ya uendeshaji wa michuano ya CECAFA hapa nchini iliwasilisha malalamiko yake kwa CECAFA kutokana na utovu wa nidhamu uliooneshwa na Kocha wa Gor Mahia Frank Nutall pamoja na timu yake kwa kutumia mlango ambao hawakutakiwa kuingilia na kutoka vyumbani ambapo CECAFA imewapa onyo kali na kutakiwa kuacha tabia walizozionesha katika michezo iliyobakia.
0 comments:
Post a Comment