Vyama vya Siasa 21 vinavyotarajiwa kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani baadaye mwaka huu vimesaini Maadili ya uchaguzi yatakayotumika wakati wa kampeni, kupiga kura na wakati wa kutangaza matokeo.Maadili hayo yanayohusisha Serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Vyama vya Siasa yalisainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dr. Florence Turuka, Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva na Wawakilishi wa vyama vya Siasa 21 nchini.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume hiyo amesema Chama
cha Wananchi (CUF) hakikusaini Maadili hayo kutokana na kuwa na kazi
nyingine lakini akasisitiza kuwa Chama hicho kitasaini Maadili hayo
wakati wowote.Akifafanua kuhusu Maadili hayo, Jaji Lubuva alisema
Maadili yanapaswa kuanza kutumika rasmi Agosti 22 mwaka huu wakati
kampeni za uchaguzi zitakapoanza, katika kipindi cha kupiga kura na
wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo.
Alisema Maadili hayo
pia yatahusu wajibu wa vyama vya siasa na wagombea na mambo yasiyotakiwa
kufanywa na vyama vya siasa na wagombea. Maadili pia yatahusu masuala
yanayotakiwa kufanywa na yasiyotakiwa kufanywa wakati wa kupiga
kura.Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa maadili yaliyosainiwa pia yatahusu
maadili kwa Tume ya Uchaguzi yaani mambo yanayotakiwa na yasiyotakiwa
kufanywa na Tume hiyo. Aidha, maadili hayo yatahusu mambo yanayotakiwa
na yasiyotakiwa kufanywa na watendaji wa serikali katika kipindi chote
cha uchaguzi.
0 comments:
Post a Comment