Kiongozi wa Chama cha ACT -Wazalendo Zitto Kabwe, akishiriki kuzika miili ya watu walioungua kwa moto uliotokana na ajali jana.
Umati wa wananchi
Mamia
ya wakazi wa wilaya za Kilosa na Kilombero wamejitokeza katika
mazisha ya pamoja ya watu kumi na tano kati ya kumi na tisa
waliofariki katika ajali ya basi ya nganga ambalo liligongana na fuso
kisha kuwaka moto katika eneo la Iyovi na kuzikwa katika kaburi la
pamoja kwenye makaburi ya Msamvu ruaha wilayani kilosa mkoani Morogoro.
Wakizungumza
kwa niaba ya serikali mkuu wa wilaya ya kilosa Bw John Henjewele
amesema serikali imewalazimu kufanya mazishi ya pamoja ya watu
waliofariki kwenye ajali hiyo ambao miili yao haijatambulika na kwamba
serikali itaendelea na zoezi la ukaguzi wa magari amkoani wa Morogoro
ili kudhibiti ajali za mara kwa mara na kupoteza maisha ya watu huku
wengine wakiachwa na vilemalema vya maisha ambapo mkuu wa wilaya ya
kilombero Bw Lephy Gembe amewataka wananchi kuwa na uvumilivu katika
msiba mkubwa walioupata.
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya ruaha Rahel Nyangasa amesema wamepokea
msiba huo kwa masikitiko makubwa kwani umekuwa ni pigo kubwa kwa wakazi
wa wilaya hizo huku ndugu na waombolezaji wakisema msiba huo
siwakusahaulika kwani umewastua sana ambapo naye muinjilisti wa kanisa
la kiinjili la kilutheri Issaya Chura akiomba serikali kuendelea
kukabiliana na madereva wabovu.
0 comments:
Post a Comment