Mshambuliaji wa
klabu ya Arsenal Danny Welbeck atakuwa nje ya Uwanja mpaka mwezi Disemba
baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye Goti .
Arsenal imeeleza kuwa matibabu kwenye Goti hilo hayakwenda vizuri na Wiki iliyopita ikaamuliwa afanyiwe operesheni.

Hili ni pigo kubwa kwa Arsenal ambayo haikusajili mshambuliaji . Dirisha la usajili la kiangazi lilifungwa jumanne iliyopita.
Mfaransa Oliver Giroud anabaki kuwa mshambuliaji pekee wa kutumainiwa katika kikosi hicho.
0 comments:
Post a Comment